1. Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.
2. Na wana wa Kohathi; Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.
3. Na wana wa Amramu; Haruni, na Musa, na Miriamu. Na wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.
4. Eleazari akamzaa Finehasi; na Finehasi akamzaa Abishua;
5. na Abishua akamzaa Buki; na Buki akamzaa Uzi;
6. na Uzi akamzaa Zerahia; na Zerahia akamzaa Merayothi,