1. Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.
2. Na wana wa Kohathi; Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.
3. Na wana wa Amramu; Haruni, na Musa, na Miriamu. Na wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.
4. Eleazari akamzaa Finehasi; na Finehasi akamzaa Abishua;
5. na Abishua akamzaa Buki; na Buki akamzaa Uzi;
6. na Uzi akamzaa Zerahia; na Zerahia akamzaa Merayothi,
7. na Merayothi akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu;
8. na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Ahimaasi;
9. na Ahimaasi akamzaa Azaria; na Azaria akamzaa Yohana;
10. na Yohana akamzaa Azaria (ndiye huyo aliyefanya kazi ya ukuhani katika nyumba aliyoijenga Sulemani huko Yerusalemu)
11. na Azaria akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu;