1 Nya. 5:12-21 Swahili Union Version (SUV)

12. Yoeli, alikuwa mkuu wao, na wa pili Shafamu, na Yanai, na Shafati, katika Bashani;

13. na ndugu zao wa mbari za baba zao; Mikaeli, na Meshulamu, na Sheba, na Yorai, na Yakani, na Zia, na Eberi, watu saba.

14. Hao ndio wana wa Abihaili, mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yehishai, mwana wa Yado, mwana wa Buzi;

15. Ahi, mwana wa Abdieli, mwana wa Guni, alikuwa mkuu wa mbari za baba zao.

16. Nao wakakaa huko Gileadi, katika Bashani, na katika miji yake, na katika viunga vyote vya Sharoni, hata kufika mipakani mwake.

17. Hao wote walihesabiwa kwa nasaba, katika siku za Yothamu, mfalme wa Yuda, na siku za Yeroboamu, mfalme wa Israeli.

18. Wana wa Reubeni, na Wagadi, na nusu-kabila ya Manase, watu mashujaa, wawezao kuchukua ngao na upanga, na kupiga upinde, wenye ustadi katika kupigana vita, walikuwa watu arobaini na nne elfu mia saba na sitini, walioweza kwenda vitani.

19. Nao wakapigana vita na Wahajiri; na Yeturi, na Nafishi, na Nodabu.

20. Wakapata msaada juu yao, nao Wahajiri walitiwa mikononi mwao, na wote waliokuwa pamoja nao; kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani; naye akayatakabali maombi yao, kwa sababu walimtumaini yeye.

21. Wakateka nyara ng’ombe zao, na ngamia zao hamsini elfu, na kondoo zao mia mbili na hamsini elfu, na punda zao elfu mbili; na watu mia elfu.

1 Nya. 5