21. Wana wa Shela, mwana wa Yuda; Eri, babaye Leka, na Laada, babaye Maresha, na jamaa zao wa mbari ya wafuma nguo za kitani safi, wa mbari ya Ashbea;
22. na Yokimu, na watu wa Kozeba, na Yoashi, na Sarafi waliokuwa na mamlaka katika Moabu, na Yashubi-lehemu. Na taarifa hizi ni za zamani sana.
23. Hao ndio waliokuwa wafinyanzi, na wenyeji wa Netaimu na Gedera; ndipo walipokaa pamoja na mfalme ili kufanya kazi yake.
24. Wana wa Simeoni; Yemueli, na Yamini, na Yakini, na Sohari, na Shauli;
25. na mwanawe huyo ni Shalumu, na mwanawe huyo ni Mibsamu, na mwanawe huyo ni Mishma.
26. Na wana wa Mishma; mwanawe huyo ni Hamueli, na mwanawe huyo ni Zakuri, na mwanawe huyo ni Shimei.
27. Naye Shimei alikuwa na wana wa kiume kumi na sita, na wana wa kike sita; walakini nduguze walikuwa hawana watoto wengi, tena jamaa yao yote haikuongezeka sana kwa mfano wa wana wa Yuda.
28. Nao wakakaa huko Beer-sheba, na Molada, na Hasar-shuali;
29. na huko Bilha, na Esemu, na Toladi;
30. na huko Bethueli, na Horma, na Siklagi;
31. na huko, Beth-markabothi, na Hasar-susimu, na Bethbiri, na Shaaraimu. Hiyo ndiyo miji yao hata wakati wa kumiliki Daudi.
32. Na vijiji vyao vilikuwa Etamu, na Aini, na Rimoni, na Tokeni, na Ashani, miji mitano,