16. Na wana wa Yehoyakimu ni hawa; mwanawe Yekonia, na mwanawe Sedekia.
17. Na wana wa Yekonia, huyo aliyechukuliwa mateka; mwanawe Shealtieli,
18. na Malkiramu, na Pedaya, na Shenazari, na Yekamia, na Hoshama, na Nedabia.
19. Na wana wa Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na Shelomithi alikuwa umbu lao;
20. na Hashuba, na Oheli, na Berekia, na Hasadia, na Yushab-Hesedi, watu watano.