14. na mwanawe huyo ni Amoni; na mwanawe huyo ni Yosia.
15. Na wana wa Yosia walikuwa hawa; Yohana mzaliwa wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia, wa nne Shalumu.
16. Na wana wa Yehoyakimu ni hawa; mwanawe Yekonia, na mwanawe Sedekia.
17. Na wana wa Yekonia, huyo aliyechukuliwa mateka; mwanawe Shealtieli,
18. na Malkiramu, na Pedaya, na Shenazari, na Yekamia, na Hoshama, na Nedabia.
19. Na wana wa Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na Shelomithi alikuwa umbu lao;
20. na Hashuba, na Oheli, na Berekia, na Hasadia, na Yushab-Hesedi, watu watano.
21. Na wana wa Hanania; Pelatia na Yeshaya; na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.
22. Na wana wa Shekania ni hawa; Shemaya, na wana wa Shemaya; Hatushi, na Igali, na Baria, na Nearia, na Shafati, watu sita.