10. Na mwanawe Sulemani alikuwa Rehoboamu; na mwanawe huyo alikuwa Abiya; na mwanawe huyo ni Asa; na mwanawe huyo ni Yehoshafati;
11. na mwanawe huyo ni Yehoramu; na mwanawe huyo ni Ahazia; na mwanawe huyo ni Yoashi;
12. na mwanawe huyo ni Amazia; na mwanawe huyo ni Uzia; na mwanawe huyo ni Yothamu;
13. na mwanawe huyo ni Ahazi; na mwanawe huyo ni Hezekia; na mwanawe huyo ni Manase;
14. na mwanawe huyo ni Amoni; na mwanawe huyo ni Yosia.
15. Na wana wa Yosia walikuwa hawa; Yohana mzaliwa wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia, wa nne Shalumu.
16. Na wana wa Yehoyakimu ni hawa; mwanawe Yekonia, na mwanawe Sedekia.
17. Na wana wa Yekonia, huyo aliyechukuliwa mateka; mwanawe Shealtieli,
18. na Malkiramu, na Pedaya, na Shenazari, na Yekamia, na Hoshama, na Nedabia.
19. Na wana wa Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na Shelomithi alikuwa umbu lao;
20. na Hashuba, na Oheli, na Berekia, na Hasadia, na Yushab-Hesedi, watu watano.
21. Na wana wa Hanania; Pelatia na Yeshaya; na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.
22. Na wana wa Shekania ni hawa; Shemaya, na wana wa Shemaya; Hatushi, na Igali, na Baria, na Nearia, na Shafati, watu sita.
23. Na wana wa Nearia; Elioenai, na Hezekia, na Azrikamu, watu watatu.
24. Na wana wa Elioenai; Hodavia, na Eliashibu, na Pelaya, na Akubu, na Yohana, na Delaya, na Anani, watu saba.