1. Basi hawa ndio wana wa Daudi, aliozaliwa huko Hebroni; Amnoni, mzaliwa wa kwanza, mwana wa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili, Danieli, wa Abigaili, Mkarmeli;
2. wa tatu, Absalomu, mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, mwana wa Hagithi;
3. wa tano, Shefatia, wa Abitali; wa sita, Ithreamu, kwa Egla, mkewe.
4. Sita alizaliwa huko Hebroni; na huko akamiliki miaka saba na miezi sita; na huko Yerusalemu akamiliki miaka thelathini na mitatu.
5. Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu;
6. na Ibhari, na Elishua, na Elipeleti;
7. na Noga, na Nefegi, na Yafia;
8. na Elishama, na Eliada, na Elifeleti, watu kenda.
9. Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wana wa masuria; na Tamari alikuwa umbu lao.
10. Na mwanawe Sulemani alikuwa Rehoboamu; na mwanawe huyo alikuwa Abiya; na mwanawe huyo ni Asa; na mwanawe huyo ni Yehoshafati;
11. na mwanawe huyo ni Yehoramu; na mwanawe huyo ni Ahazia; na mwanawe huyo ni Yoashi;
12. na mwanawe huyo ni Amazia; na mwanawe huyo ni Uzia; na mwanawe huyo ni Yothamu;