13. Nao wakatupiwa kura kwa ajili ya kila lango, wadogo sawasawa na wakubwa, kwa kadiri ya mbari za baba zao.
14. Kura ya mashariki ya lango ikamwangukia Meshelemia. Ndipo wakamtupia kura Zekaria mwanawe, mshauri mwenye busara; na kura yake ikamtokea ya kaskazini.
15. Ya Obed-edomu ya kusini; na ya wanawe nyumba ya akiba.
16. Ya Shupimu na Hosa upande wa magharibi, langoni pa Shalekethi, hapo penye daraja ya kupandia, ulinzi kwa ulinzi.
17. Upande wa mashariki walikuwapo Walawi sita, kaskazini wanne kila siku, kusini wanne kila siku, na wa nyumba ya akiba wawili wawili.
18. Penye Parbari upande wa magharibi, walikuwapo wanne darajani, na wawili huko Parbari.
19. Hizo ndizo zamu za mabawabu; wa wana wa Wakora, na wa wana wa Merari.
20. Na katika Walawi; Ahia alikuwa juu ya hazina za nyumba ya Mungu, na juu ya hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.
21. Wana wa Ladani; wana wa Wagershoni waliokuwa wa Ladani; wakuu wa mbari za mababa waliokuwa wa Ladani, Mgershoni; Yehieli.
22. Wana wa Yehieli; Zethamu, na Yoeli nduguye, juu ya hazina za nyumba ya BWANA.