1 Nya. 25:4-19 Swahili Union Version (SUV)

4. Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi;

5. hao wote ndio wana wa Hemani, mwonaji wa mfalme, kwa maneno ya Mungu, ili kuinua pembe. Naye Mungu akampa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.

6. Hao wote waliamriwa na baba yao, waimbe nyumbani mwa BWANA, wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, kwa utumishi wa nyumba ya Mungu; Asafu, Yeduthuni, na Hemani wakiwa wanaamriwa na mfalme.

7. Na hesabu yao, pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia BWANA, wote waliokuwa wastadi, walikuwa mia mbili na themanini na wanane.

8. Wakatupiwa kura ya ulinzi wao, sawasawa wote, mdogo kwa mkubwa, mwalimu kwa mwanafunzi.

9. Kura ya kwanza ikamtokea Yusufu, kwa Asafu; ya pili Gedalia; yeye na nduguze na wanawe, kumi na wawili;

10. ya tatu Zakuri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

11. ya nne Seri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

12. ya tano Nethania, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

13. ya sita Bukia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

14. ya saba Asharela, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

15. ya nane Yeshaya, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

16. ya kenda Matania wanawe na nduguze, kumi na wawili;

17. ya kumi Shimei, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

18. ya kumi na moja Uzieli, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

19. ya kumi na mbili Hashabia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Nya. 25