3. Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikapata thelathini na nane elfu.
4. Katika hao ishirini na nne elfu walikuwa wa kusimamia kazi ya nyumba ya BWANA; na sita elfu walikuwa maakida na makadhi;
5. na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu BWANA kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.
6. Basi Daudi akawagawanya kuwa zamu zao sawasawa na wana wa Lawi; Gershoni, Kohathi, na Merari.
7. Wa Wagershoni; Ladani, na Shimei.
8. Wana wa Ladani; Yehieli mkuu wao, na Zethamu, na Yoeli, watu watatu.
9. Wana wa Shimei; Shelomothi, na Hazieli, na Harani, watatu. Hao walikuwa vichwa vya mbari za baba za Ladani.
10. Na wana wa Shimei; Yahathi, na Zina, na Yeushi, na Beria. Hao wanne walikuwa wana wa Shimei.
11. Naye Yahathi alikuwa mkubwa wao, na Zina alikuwa wa pili; lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; basi wakawa mbari ya baba kwa kuhesabiwa pamoja.
12. Wana wa Kohathi; Amramu, Ishari, Hebroni, na Uzieli, watu wanne.