1. Basi Daudi alikuwa mzee, ameshiba siku; akamtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme juu ya Israeli.
2. Akawakusanya wakuu wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi.
3. Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikapata thelathini na nane elfu.
4. Katika hao ishirini na nne elfu walikuwa wa kusimamia kazi ya nyumba ya BWANA; na sita elfu walikuwa maakida na makadhi;
5. na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu BWANA kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.
6. Basi Daudi akawagawanya kuwa zamu zao sawasawa na wana wa Lawi; Gershoni, Kohathi, na Merari.
7. Wa Wagershoni; Ladani, na Shimei.
8. Wana wa Ladani; Yehieli mkuu wao, na Zethamu, na Yoeli, watu watatu.