1 Nya. 21:26-28 Swahili Union Version (SUV)

26. Kisha Daudi akamjengea BWANA madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akamlingana BWANA; naye akamwitikia kutoka mbinguni kwa moto juu ya madhabahu hiyo ya sadaka ya kuteketezwa.

27. BWANA naye akamwamuru malaika; naye akaurudisha upanga wake alani mwake tena.

28. Wakati huo, Daudi alipoona ya kwamba BWANA amemwitikia katika kiwanja cha Arauna, Myebusi, ndipo hutoa dhabihu huko.

1 Nya. 21