7. Na wana wa Karmi; Akani, yule mwenye kutaabisha Israeli, aliyekosa katika kitu kilichowekwa wakfu.
8. Na wana wa Ethani; Azaria.
9. Tena wana wa Hesroni aliozaliwa; Yerameeli, na Ramu, na Kalebu.
10. Na Ramu akamzaa Aminadabu; na Aminadabu akamzaa Nashoni, mkuu wa wana wa Yuda;
11. na Nashoni akamzaa Salmoni; na Salmoni akamzaa Boazi;
12. na Boazi akamzaa Obedi; na Obedi akamzaa Yese;
13. na Yese akamzaa Eliabu, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama;
14. na wa nne Nethaneli, na wa tano Radai;
15. na wa sita Ozemu, na wa saba Daudi;
16. na maumbu yao ni Seruya, na Abigaili. Na wana wa Seruya walikuwa, Abishai, na Yoabu, na Asaheli; hao watatu.
17. Na Abigaili akamzaa Amasa; na babaye Amasa ni Yetheri, Mwishmaeli.
18. Basi Kalebu, mwana wa Hesroni, akazaliwa wana na mkewe Azubu, na Yeriothi, na hawa ndio wanawe wa kiume; Yesheri, na Shobabu, na Ardoni.
19. Akafa Azuba, naye Kalebu akamtwaa Efrathi, aliyemzalia Huri.
20. Naye Huri akamzaa Uri; na Uri akamzaa Besaleli.
21. Na baadaye Hesroni akamwingilia binti wa Makiri, babaye Gileadi; ambaye alimtwaa alipokuwa mwenye miaka sitini; naye akamzalia Segubu.
22. Na Segubu akamzaa Yairi, aliyekuwa mwenye miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.