51. Salma, babaye Bethlehemu; na Harefu, babaye Beth-gaderi.
52. Naye Shobali, babaye Kiriath-Yearimu, alikuwa na wana; Haroe, na nusu ya Wamenuhothi.
53. Na jamaa za Kiriath-Yearimu; Waithri, na Waputhi, na Washumathi, na Wamishrai; katika hao walitoka Wasorathi, na Waeshtaoli.
54. Na wana wa Salma; Bethlehemu, na Wanetofathi, Atroth-beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi, na Wazori.