1 Nya. 2:45-55 Swahili Union Version (SUV)

45. Na mwana wake Shamai alikuwa Maoni; na Maoni alikuwa babaye Bethsuri.

46. Naye Efa, suria yake Kalebu, alimzaa Harani, na Mosa, na Gazezi; naye Harani akamzaa Gazezi.

47. Na wana wa Yadai; Regemu, na Yothamu, na Geshani, na Peleti, na Efa, na Shaafu.

48. Naye Maaka, suria yake Kalebu, akamzalia Sheberi, na Tirhana.

49. Tena akamzaa Shaafu, babaye Madmana; na Sheva babaye Makbena; na babaye Gibea; naye binti Kalebu alikuwa Aksa.

50. Hao walikuwa wana wa Kalebu. Wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi; Shobali, babaye Kiriath-Yearimu;

51. Salma, babaye Bethlehemu; na Harefu, babaye Beth-gaderi.

52. Naye Shobali, babaye Kiriath-Yearimu, alikuwa na wana; Haroe, na nusu ya Wamenuhothi.

53. Na jamaa za Kiriath-Yearimu; Waithri, na Waputhi, na Washumathi, na Wamishrai; katika hao walitoka Wasorathi, na Waeshtaoli.

54. Na wana wa Salma; Bethlehemu, na Wanetofathi, Atroth-beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi, na Wazori.

55. Na jamaa za waandishi waliokaa Yabesi; Watirathi, na Washimeathi, na Wasukathi. Hao ndio Wakeni, waliotoka kwake Hamathi, babaye mbari ya Rekabu.

1 Nya. 2