33. Na wana wa Yonathani; Pelethi, na Zaza. Hao ndio wana wa Yerameeli.
34. Basi huyo Sheshani alikuwa hana wana wa kiume, ila binti. Naye Sheshani alikuwa na mtumwa, Mmisri, jina lake akiitwa Yarha.
35. Basi akamwoza binti yake aolewe na Yarha, mtumwa wake; naye akamzalia Atai.
36. Na Atai akamzaa Nathani; na Nathani akamzaa Zabadi;
37. na Zabadi akamzaa Eflali; na Eflali akamzaa Obedi;
38. na Obedi akamzaa Yehu; na Yehu akamzaa Azaria;