30. Na wana wa Nadabu; Seledi, na Apaimu; walakini Seledi alikufa hana watoto.
31. Na wana wa Apaimu; Ishi. Na wana wa Ishi; Sheshani. Na wana wa Sheshani; Alai.
32. Na wana wa Yada, nduguye Shamai; Yetheri, na Yonathani; naye Yetheri akafa hana watoto.
33. Na wana wa Yonathani; Pelethi, na Zaza. Hao ndio wana wa Yerameeli.
34. Basi huyo Sheshani alikuwa hana wana wa kiume, ila binti. Naye Sheshani alikuwa na mtumwa, Mmisri, jina lake akiitwa Yarha.
35. Basi akamwoza binti yake aolewe na Yarha, mtumwa wake; naye akamzalia Atai.