25. Na wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa Ramu, mzaliwa wa kwanza, na Buna, na Oreni, na Ozemu; kwa Ahiya.
26. Naye Yerameeli alikuwa na mke mwingine, jina lake Atara; yeye alikuwa mamaye Onamu.
27. Na wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, na Yamini, na Ekeri.
28. Na wana wa Onamu walikuwa Shamai, na Yada; na wana wa Shamai; Nadabu, na Abishuri.