2. na Dani, na Yusufu, na Benyamini, na Naftali, na Gadi, na Asheri.
3. Wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela; ambao hao watatu alizaliwa na binti Shua, Mkanaani. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa BWANA; naye akamwua.
4. Na Tamari, mkwewe, akamzalia Peresi, na Zera. Wana wote wa Yuda ni watano.
5. Wana wa Peresi; Hesroni, na Hamuli.
6. Na wana wa Zera; Zabdi, na Ethani, na Hemani, na Kalkoli, na Darda; hao wote ni watano.
7. Na wana wa Karmi; Akani, yule mwenye kutaabisha Israeli, aliyekosa katika kitu kilichowekwa wakfu.
8. Na wana wa Ethani; Azaria.
9. Tena wana wa Hesroni aliozaliwa; Yerameeli, na Ramu, na Kalebu.