18. Basi Kalebu, mwana wa Hesroni, akazaliwa wana na mkewe Azubu, na Yeriothi, na hawa ndio wanawe wa kiume; Yesheri, na Shobabu, na Ardoni.
19. Akafa Azuba, naye Kalebu akamtwaa Efrathi, aliyemzalia Huri.
20. Naye Huri akamzaa Uri; na Uri akamzaa Besaleli.
21. Na baadaye Hesroni akamwingilia binti wa Makiri, babaye Gileadi; ambaye alimtwaa alipokuwa mwenye miaka sitini; naye akamzalia Segubu.
22. Na Segubu akamzaa Yairi, aliyekuwa mwenye miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.
23. Na Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi, pamoja na Kenathi na miji yake, jumla yote miji sitini. Hao wote ni wana wa Makiri, babaye Gileadi.
24. Tena, baada ya kufa kwake Hesroni huko Kalebu-Efrata, ndipo Abia, mkewe Hesroni, alipomzalia Ashuri, babaye Teboa.