1 Nya. 2:1-13 Swahili Union Version (SUV)

1. Hawa ndio wana wa Israeli; Reubeni, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni;

2. na Dani, na Yusufu, na Benyamini, na Naftali, na Gadi, na Asheri.

3. Wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela; ambao hao watatu alizaliwa na binti Shua, Mkanaani. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa BWANA; naye akamwua.

4. Na Tamari, mkwewe, akamzalia Peresi, na Zera. Wana wote wa Yuda ni watano.

5. Wana wa Peresi; Hesroni, na Hamuli.

6. Na wana wa Zera; Zabdi, na Ethani, na Hemani, na Kalkoli, na Darda; hao wote ni watano.

7. Na wana wa Karmi; Akani, yule mwenye kutaabisha Israeli, aliyekosa katika kitu kilichowekwa wakfu.

8. Na wana wa Ethani; Azaria.

9. Tena wana wa Hesroni aliozaliwa; Yerameeli, na Ramu, na Kalebu.

10. Na Ramu akamzaa Aminadabu; na Aminadabu akamzaa Nashoni, mkuu wa wana wa Yuda;

11. na Nashoni akamzaa Salmoni; na Salmoni akamzaa Boazi;

12. na Boazi akamzaa Obedi; na Obedi akamzaa Yese;

13. na Yese akamzaa Eliabu, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama;

1 Nya. 2