1 Nya. 12:5-14 Swahili Union Version (SUV)

5. Eluzai, na Yerimothi, na Bealia, na Shemaria, na Shefatia Mharufi;

6. Elkana, na Ishia, na Azaleli, na Yoezeri, na Yashobeamu, Wakora;

7. na Yoela, na Zebadia, wana wa Yerohamu, wa Gedori.

8. Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, waume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima;

9. Ezeri mkubwa wao, Obadia wa pili, Eliabu wa tatu;

10. Mishmana wa nne, Yeremia wa tano;

11. Atai wa sita, Elieli wa saba;

12. Yohana wa nane, Elzabadi wa kenda;

13. Yeremia wa kumi, Makbanai wa kumi na moja.

14. Hao wa wana wa Gadi walikuwa maakida wa jeshi, yeye aliyekuwa mdogo amelingana na mia, na yeye aliyekuwa mkuu, na elfu.

1 Nya. 12