1 Nya. 11:19-38 Swahili Union Version (SUV)

19. akasema, Mungu wangu apishe mbali, nisifanye hivi; je! Ninywe damu ya watu hao waliohatirisha nafsi zao? Maana kwa hatari ya nafsi zao wameyaleta. Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.

20. Tena Abishai, nduguye Yoabu, alikuwa mkuu wa wale watatu; kwa kuwa aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua; akawa na jina kati ya wale watatu.

21. Katika wale watatu yeye alikuwa mwenye heshima kuliko hao wawili, akawa akida wao; ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu.

22. Tena, Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari, wa Kabseeli, aliyekuwa amefanya mambo makuu, ndiye aliyewaua simba wakali wawili wa Moabu; pia akashuka, akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theluji.

23. Huyo akamwua Mmisri, mtu mrefu sana, aliyekuwa wa dhiraa tano urefu wake; na yule Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi; lakini yeye akamshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe.

24. Mambo hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, akawa na jina kati ya wale mashujaa watatu.

25. Tazama, alikuwa mwenye heshima kuliko wale thelathini, ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu; naye Daudi akamweka juu ya walinzi wake.

26. Tena hawa ndio mashujaa wa majeshi ya askari; Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethlehemu;

27. Shama Mharodi, Helesi Mpeloni;

28. Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi, Abiezeri Mwanathothi;

29. Sibekai Mhushathi, Salmoni Mwahohi;

30. Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana Mnetofathi;

31. Itai mwana wa Ribai wa Gibea wa wana wa Benyamini, Benaya Mpirathoni;

32. Hurai wa vijito vya Gaashi, Abieli Mwaibathi;

33. Azmawethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni;

34. wana wa Yasheni Mgiloni, Yonathani mwana wa Shama Mharari;

35. Ahiamu mwana wa Sharari Mharari, Elifeleti mwana wa Ahasbai; Heferi

36. Mmaakathi, Ahia Mpeloni;

37. Hezro Mkarmeli, Paarai mwana wa Ezbai Mwarki;

38. Yoeli nduguye Nathani, Mibhari mwana wa Hagri;

1 Nya. 11