9. Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani.
10. Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
11. Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi,
12. na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori.
13. Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi;
14. na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi;