1 Nya. 1:48-54 Swahili Union Version (SUV)

48. Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akamiliki badala yake.

49. Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akamiliki badala yake.

50. Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akamiliki badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu.

51. Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi;

52. na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni;

53. na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari;

54. na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.

1 Nya. 1