45. Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akamiliki badala yake.
46. Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akamiliki badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi.
47. Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akamiliki badala yake.
48. Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akamiliki badala yake.