1 Nya. 1:32-42 Swahili Union Version (SUV)

32. Na wana wa Ketura, suria yake Ibrahimu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani.

33. Na wana wa Midiani; Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote ndio wana wa Ketura.

34. Na Ibrahimu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli.

35. Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora.

36. Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki.

37. Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza.

38. Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani.

39. Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni umbu lake Lotani.

40. Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana.

41. Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani.

42. Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani.

1 Nya. 1