27. na Abramu, naye ndiye Ibrahimu.
28. Wana wa Ibrahimu; Isaka, na Ishmaeli.
29. Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu;
30. na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema;
31. na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
32. Na wana wa Ketura, suria yake Ibrahimu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani.
33. Na wana wa Midiani; Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote ndio wana wa Ketura.
34. Na Ibrahimu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli.
35. Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora.
36. Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki.
37. Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza.
38. Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani.
39. Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni umbu lake Lotani.