20. Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera;
21. na Hadoramu, na Uzali, na Dikla;
22. na Obali, na Abimaeli, na Sheba;
23. na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
24. Shemu, na Arfaksadi, na Sala;
25. na Eberi, na Pelegi, na Reu;
26. na Serugi, na Nahori, na Tera;
27. na Abramu, naye ndiye Ibrahimu.
28. Wana wa Ibrahimu; Isaka, na Ishmaeli.
29. Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu;
30. na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema;
31. na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
32. Na wana wa Ketura, suria yake Ibrahimu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani.