1 Nya. 1:2-19 Swahili Union Version (SUV)

2. na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi;

3. na Henoko, na Methusela, na Lameki;

4. na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi.

5. Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.

6. Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.

7. Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani.

8. Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.

9. Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani.

10. Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.

11. Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi,

12. na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori.

13. Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi;

14. na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi;

15. na Mhivi, na Mwarki, na Msini;

16. na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi.

17. Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.

18. Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi.

19. Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani.

1 Nya. 1