13. Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi;
14. na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi;
15. na Mhivi, na Mwarki, na Msini;
16. na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi.
17. Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.
18. Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi.
19. Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani.
20. Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera;
21. na Hadoramu, na Uzali, na Dikla;
22. na Obali, na Abimaeli, na Sheba;
23. na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
24. Shemu, na Arfaksadi, na Sala;
25. na Eberi, na Pelegi, na Reu;
26. na Serugi, na Nahori, na Tera;