10. Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
11. Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi,
12. na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori.
13. Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi;
14. na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi;
15. na Mhivi, na Mwarki, na Msini;
16. na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi.
17. Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.