4. Je! Hatuna uwezo wa kula na kunywa?
5. Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?
6. Au je! Ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo wa kutokufanya kazi?
7. Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi?
8. Je! Ninanena hayo kwa kibinadamu? Au torati nayo haisemi yayo hayo?