2. Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, lakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana ninyi ndinyi muhuri ya utume wangu katika Bwana.
3. Hilo ndilo jawabu langu kwa wale wanaoniuliza.
4. Je! Hatuna uwezo wa kula na kunywa?
5. Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?
6. Au je! Ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo wa kutokufanya kazi?
7. Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi?