19. Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.
20. Na tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili.
21. Basi, mtu ye yote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu;
22. kwamba ni Paulo, au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu;
23. nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.