7. Maana sipendi kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraji kukaa kwenu muda kidogo, Bwana akinijalia.
8. Lakini nitakaa Efeso hata Pentekoste;
9. kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.
10. Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo hofu; maana anaifanya kazi ya Bwana vile vile kama mimi mwenyewe;
11. basi mtu ye yote asimdharau, lakini msafirisheni kwa amani, ili aje kwangu; maana ninamtazamia pamoja na ndugu zetu.
12. Lakini kwa habari za Apolo, ndugu yetu, nalimsihi sana aende kwenu pamoja na hao ndugu; ambaye si mapenzi yake kwenda sasa; lakini atakuja atakapopata nafasi.
13. Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari.
14. Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.
15. Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa Stefana kwamba ni malimbuko ya Akaya, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumu watakatifu);
16. watiini watu kama hawa, na kila mtu afanyaye kazi pamoja nao, na kujitaabisha.
17. Nami nafurahi kwa sababu ya kuja kwao Stefana na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikirimia kwa wingi yale niliyopungukiwa kwenu.
18. Maana wameniburudisha roho yangu, na roho zenu pia; basi wajueni sana watu kama hao.
19. Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Priska wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao.