1 Kor. 14:31-40 Swahili Union Version (SUV)

31. Kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja, ili wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe.

32. Na roho za manabii huwatii manabii.

33. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.

34. Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.

35. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.

36. Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?

37. Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.

38. Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga.

39. Kwa ajili ya hayo, ndugu, takeni sana kuhutubu, wala msizuie kunena kwa lugha.

40. Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.

1 Kor. 14