1 Kor. 12:14-22 Swahili Union Version (SUV)

14. Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.

15. Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo?

16. Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo?

17. Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa?

18. Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka.

19. Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?

20. Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja.

21. Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi.

22. Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi.

1 Kor. 12