1 Kor. 10:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;

2. wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;

3. wote wakala chakula kile kile cha roho;

4. wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.

5. Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.

6. Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.

7. Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.

8. Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.

1 Kor. 10