Hivyo ikamalizika kazi yote Sulemani mfalme aliyoifanya katika nyumba ya BWANA. Sulemani akaviingiza vile vitu alivyovitakasa Daudi baba yake, yaani, fedha, na dhahabu, na vyombo; akavitia ndani ya hazina za nyumba ya BWANA.