1 Fal. 6:9-14 Swahili Union Version (SUV)

9. Basi ndivyo alivyoijenga nyumba, akaimaliza; akaifunika nyumba kwa boriti na mbao za mwerezi.

10. Akavijenga vyumba mbavuni mwa nyumba yote, kwenda juu kwake kila kimoja kilikuwa mikono mitano; vikaitegemea nyumba kwa boriti za mwerezi.

11. Neno la BWANA likamjia Sulemani, kusema,

12. Katika habari ya nyumba hii unayoijenga, kama ukienda katika sheria zangu, na kuzifanya hukumu zangu, na kuzishika amri zangu zote na kwenda katika hizo; ndipo nitakapolithibitisha neno langu kwako, nililomwambia Daudi baba yako.

13. Nami nitakaa katikati ya wana wa Israeli, wala sitawaacha watu wangu Israeli.

14. Basi Sulemani akaijenga hiyo nyumba akaimaliza.

1 Fal. 6