1 Fal. 4:11-16 Swahili Union Version (SUV)

11. Mwana wa Abinadabu katika Nafath-dori yote; ndiye aliyekuwa naye Tafathi binti Sulemani kuwa mke wake.

12. Baana mwana wa Ahiludi, katika Taanaki na Megido, na Beth-sheani yote, iliyo kando ya Sarethani, chini ya Yezreeli, tangu Beth-sheani mpaka Abel-mehola, hata kupita Yokmeamu.

13. Mwana wa Geberi katika Ramoth-gileadi; na kwake ilikuwa miji ya Yairi mwana wa Manase iliyomo Gileadi; na kwake ilikuwa wilaya ya Argobu, iliyomo Bashani, miji mikubwa sitini yenye kuta na makomeo ya shaba.

14. Ahinadabu mwana wa Ido, katika Mahanaimu.

15. Ahimaasi, katika Naftali; naye ndiye aliyemwoa Basemathi binti Sulemani.

16. Baana mwana wa Hushai, katika Asheri na Bealothi.

1 Fal. 4