Na yule nabii aliyemrudisha njiani alipopata habari, akasema; Ndiye yule mtu wa Mungu, aliyeiasi kauli ya BWANA; kwa hiyo BWANA amempambanisha na simba, simba akamrarua, akamwua, sawasawa na neno la BWANA alilomwambia.