Zekaria 4:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Yule malaika aliyeongea nami, akanijia tena, akaniamsha kama kumwamsha mtu usingizini.

2. Akaniuliza, “Unaona nini?” Nami nikamjibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu. Juu yake kuna bakuli la mafuta na taa saba, na kila moja ina mahali pa kutilia tambi saba.

3. Karibu na kinara hicho kuna miti miwili ya mzeituni; mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.”

4. Basi, nikamwuliza huyo malaika, “Bwana, vitu hivi vinamaanisha nini?”

5. Naye akanijibu, “Hujui vitu hivi vinamaanisha nini?” Nikamjibu, “Sijui bwana.”

10b. Huyo malaika akaniambia, “Hizo taa saba ni macho saba ya Mwenyezi-Mungu yaonayo kila mahali duniani.”

6. Naye akaniambia pia niseme neno hili la Mwenyezi-Mungu kumhusu Zerubabeli: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: Huwezi kushinda kwa nguvu au kwa uwezo wako mwenyewe, bali kwa msaada wa roho yangu. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.”

Zekaria 4