Zekaria 13:4-9 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Siku hiyo, kila nabii atayaonea aibu maono yake anapotabiri. Hawatavaa mavazi ya manyoya ili kudanganya watu,

5. bali kila mmoja atasema, ‘Mimi si nabii. Mimi ni mkulima tu; nimeimiliki ardhi tangu ujana wangu’.

6. Na mtu akimwuliza mmoja wao, ‘Vidonda hivi ulivyo navyo mgongoni vimetoka wapi?’ Yeye atajibu, ‘Vidonda hivi nilivipata katika nyumba ya rafiki zangu.’”

7. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi:“Amka, ee upanga!Inuka umshambulie mchungaji wangu;naam, mchungaji anayenitumikia.Mpige mchungaji na kondoo watawanyike.Nitaunyosha mkono wangu,kuwashambulia watu wadhaifu.

8. Theluthi mbili za watu katika nchi zitaangamizwa;ni theluthi moja tu itakayosalimika.

9. Theluthi hiyo moja itakayosalia,nitaijaribu na kuitakasa,kama mtu asafishavyo fedha,naam, kama ijaribiwavyo dhahabu.Hapo wao wataniomba mimi,nami nitawajibu.Nitasema, ‘Hawa ni watu wangu’,nao watasema, ‘Mwenyezi-Mungu, ndiye Mungu wetu.’”

Zekaria 13