9. Japo niliwatawanya kati ya mataifa,hata hivyo, watanikumbuka wakiwa humo.Nao pamoja na watoto wao wataishina kurudi majumbani mwao.
10. Nitawarudisha kutoka nchini Misri,nitawakusanya kutoka Ashuru;nitawaleta nchini Gileadi na Lebanoni,nao watajaa kila mahali nchini.
11. Watapitia katika bahari ya mateso,nami nitayapiga mawimbi yake,na vilindi vya maji ya mto Nili vitakauka.Kiburi cha Ashuru kitavunjwana nguvu za Misri zitatoweka.
12. Mimi nitawaimarisha watu wangu,nao watanitii na kuishi kwa kunipendeza.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”