3. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nimewaka hasira dhidi ya hao wachungaji,nami nitawaadhibu hao viongozi.Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi,nitalitunza kundi langu, ukoo wa Yuda.Nitawafanya kuwa farasi wangu hodari wa vita.
4. Kwa ukoo wa Yuda kutatokea:Watawala wa kila namna,viongozi imara kama jiwe kuu la msingi,walio thabiti kama kigingi cha hema,wenye nguvu kama upinde wa vita.
5. Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa vitaniwatawakanyaga maadui zao katika tope njiani.Watapigana kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nipo pamoja nao;nao watawaaibisha hata wapandafarasi.
6. “Watu wa Yuda nitawaimarisha;nitawaokoa wazawa wa Yosefu.Nitawarejesha makwao kwa maana nawaonea huruma,nao watakuwa kana kwamba sikuwa nimewakataa.Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao,nami nitayasikiliza maombi yao.
7. Watu wa Efraimu watakuwa kama mashujaa vitani;watajaa furaha kama waliokunywa divai.Watoto wao wataona hayo na kufurahi,watajaa furaha mioyoni kwa sababu yangu Mwenyezi-Mungu.