Zaburi 6:7-10 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Macho yangu yamechoka kwa huzuni;yamefifia kwa kutaabishwa na adui.

8. Ondokeni kwangu enyi nyote watenda maovu!Maana Mwenyezi-Mungu amesikia kilio changu.

9. Mwenyezi-Mungu amesikia ombi langu;Mwenyezi-Mungu amekubali sala yangu.

10. Maadui zangu wote wataaibika na kufadhaika;watarudi nyuma na kuaibishwa ghafla.

Zaburi 6