8. Uniongoze, ee Mwenyezi-Mungu, katika uadilifu wako,maana maadui zangu ni wengi;uiweke njia yako wazi mbele yangu.
9. Vinywani mwao hamna ukweli;mioyoni mwao wamejaa maangamizi,wasemacho ni udanganyifu wa kifo,ndimi zao zimejaa hila.
10. Uwaadhibu kwa hatia yao ee Mungu;waanguke kwa njama zao wenyewe;wafukuze nje kwa sababu ya dhambi zao nyingi,kwa sababu wamekuasi wewe.
11. Lakini wafurahi wote wanaokimbilia usalama kwako,waimbe kwa shangwe daima.Uwalinde wanaolipenda jina lako,wapate kushangilia kwa sababu yako.